HATIMAYE MKEMI ABWAGA MANYANGA YANGA
Matokeo mabovu katika michezo ya hivi karibuni yameanza kuimega klabu ya Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kuamua kuwajibika.
Wakwanza aliyejipima na kujiona hatoshi tena ni mjumbe wa kamati ya utendaji Salum Mkemi ambaye ametangaza kufanya hivyo kupitia akaunti yake ya Instagram.
"Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi
Kwa Hakika Tumepata Aibu
Kubwa
Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili
Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza"
Pamoja na hayo pia Mkemi ametumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kongwe nchini.
"Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.
Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club "YANGA " kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane."
"Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu
SALUM MKEMI
NIMENG'ATUKA"
Yanga leo wamepoteza mchezo wao wa Sportpesa Super Cup kwa kufungwa mabao 3-1 na Kakamega Home Boys ya Kenya na hivyo kuondoshwa katika mashindano hayo.

No comments