YANGA NA SIMBA ZAPANGWA KUNDI MOJA KOMBE LA KAGAME
Watani wa Jadi katika soka la Tanzania Wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na Yanga wamepangwa Kundi moja katika michuano ya kombe la Kagame linalotarajiwa kuanza jijini Dar es Salaam tarehe 29 Juni hadi tarehe 13 Julai mwaka huu.
Makundi matatu yamepangwa jijini Dar es Salaam Leo huku jumla ya timu 12 zikipangwa katika makundi hayo Simba na Yanga zenyewe zikipangwa katika Kundi C pamoja na St. George ya Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.
Mabingwa watetezi Azam FC wao wamepangwa katika Kundi A wakiwa pamoja na timu za Uganda Reps kutoka Uganda, JKU ya Zanzibar na Kator FC ya Sudan ya Kusini.
Kundi B lina timu za Rayon Sports toka Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, Lydia Ludic ya Burundi na Ports ya Djibout.
Washindi wawili wa kila Kundi watatinga hatua ya robo fainali pamoja na timu mbili zilizofanya vyema lakini hazikupata nafasi ya kwanza na ya pili maarufu kama Best Losers.
Ijumaa ya Tarehe 29 ndiyo itakua ni mechi za ufunguzi ambapo JKU itacheza na Uganda Reps saa 8 mchana huku SAA 10 Azam FC watacheza na Kator mechi hizo zikichezwa Chamazi na usiku Yanga itacheza na St. George mida ya saa 1 jioni mechi ikichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba na Yanga zitakutana katika mechi yao ya Kundi Tarehe 5 Julai uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia majira ya saa 12 jioni Ikiwa ni moja Kati ya mechi mbili za mwisho katika Kundi hilo.

No comments