USAJILI WA KWANZA WA UNAI EMERY ARSENAL, BEKI MWENYE MIAKA 34.

Kocha wa Arsenal Unai Emery ameandika historia mpya katika klabu yake hiyo mpya Kwa kumsajili beki Veterani Stephan Lichtsteiner mwenye miaka 34 kama mchezaji huru.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswis ambaye aliichezea Juventus anajiunga na Arsenal akiwa huru na atavaa jezi namba 12 na atacheza beki wa kulia sambamba na Hector Belerin.

"Stephan anajiunga na Arsenal na tunategemea atatusaidia kuongeza uongozi na 'experience' kikosini" alisema Unai Emery

Stephan alishinda ubingwa wa Italia Mara zote 7 alizoichezea Juventus akicheza mechi zaidi ya  250 na ni Nahodha wa Uswisi ambayo inashiriki katika kombe la dunia mwaka huu.

1 comment:

Powered by Blogger.