SINGIDA YALIPA KISASI KWA AFC LEOPARDS YATINGA NUSU FAINALI
Singida United imekuwa timu ya pili kutoka Tanzania kuingia nusu fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga AFC Leopards kwa mikwaju ya penati 4-2.
Mwaka jana Leopards iliitoa Singida katika hatua hiyo kwa mikwaju ya penati katika uwanja wa Uhuru na leo walima alizeti hao wamelipa kisasi.
Jana Simba iliingia nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Kariobangi Sharks kwa mikwaju ya penati 3-2.
Mlinda mlango Peter Manyika Junior aaliokoa mkwaju wa penati katika muda wa kawaida na kuifikisha Singida hatua hiyo.
Penati za Singida zilifungwa na Shafiq Batambuze, Miraji Adam, Danny Lyanga na Elinywesia Simbu huku Kenny Ally akikosa mkwaju wake.
Singida itakutana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Gor Mahia katika nusu fainali ya pili itakayofanyika siku ya Ijumaa.

No comments