USAJILI WA HAZARD NA DE GEA NDIYO CHANZO CHA ZIDANE KUONDOKA MADRID.
Vyanzo vya habari nchini Spain vimeweka wazi sababu ya kuondoka katika klabu ya Real Madrid Kwa Aliyekuwa kocha mkuu wa Mabingwa hao wa Ulaya Zenedine Zidane kuwa ni kuingiliwa katika usajili wa Eden Hazard na David De Gea.
Inasemekana Zidane alimweka Eden Hazard kama mchezaji wake wa kwanza anayetaka kumsajili kuanzia dirisha Dogo la usajili wa mwezi January lakini kikwazo kikubwa ni Rais wa timu hiyo Florentino Perez ambaye analazimisha Real Madrid imnunue kwanza Kipa namba moja wa Klabu ya Manchester United David De Gea usajili ambao utaifanya Real Madrid pengine kushindwa kumpata Eden Hazard kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kitakachotumika.
Zidane yeye hakuona umuhimu wa kusajiliwa De Gea na anaamini kipa wake namba moja Keylor Navas ambaye amempa ubingwa Mara tatu wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya anafaa kuendelea kuaminiwa lakini Perez akalazimisha na bila hiyana Zidane akaamua kuachia ngazi Alhamisi iliyopita licha ya kutwaa ubingwa wake wa tatu mfululizo akiwa na Madrid Kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

No comments