SIMBA YATANGULIA FAINALI SPORTPESA SUPER CUP

Simba imetinga fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kakamega Homeboyz kwa penati 5-4.

Simba inasubiri mshindi kati ya Singida au mabingwa watetezi Gor Mahia ambao wapo dimbani muda huu.

Bingwa wa michuano hiyo atasafiri kwenda Uingereza kucheza na timu ya Everton ambayo nayo inadhaminiwa na SportPesa.
Kiungo Rashid Juma akimtoka beki Kishuya wa Kakamega

Simba iliingia katika mchezo huo bila ya kocha wao mkuu Mfaransa Pierre Lechantre ambaye alikaa jukwaani huku sababu ya kufanya hivyo ikiwa haijatolewa ambapo msaidizi wake Masoud Djuma akiwaongoza Wekundu hao.

Wekundu hao leo walicheza vizuri kuliko mchezo wa kwanza walioshinda kwa penati pia dhidi ya Kariobangi Sharks.

Penati za Simba zilifungwa na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Shiza Kichuya na Jonas Mkude wakiwa hawajakosa hata moja.

No comments

Powered by Blogger.