DODOMA KURINDIMA NA UHAI CUP, TFF YAANIKA MAKUNDI



Michuano ya Ligi Soka ya vijana kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imepangwa kufanyika kuanzia Jumamosi hii ya Juni 9 hadi 21 katika jiji la Dodoma Kwa timu zote washiriki kucheza mechi zao Kwa mtindo wa makundi.

Timu za vijana chini ya miaka 20 kwa timu zote zilizoshiriki ligi kuu Soka Tanzania bara msimu uliomalizika Hivi karibuni na Wekundu wa Msimbazi Simba kuibuka na ubingwa na mechi za michuano hiyo zitachezwa katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kila siku zitachezwa mechi mbili saa 8 mchana na saa 10 jioni.

Bingwa wa michuano hiyo ambaye ataenda kutetea ubingwa wake ni Kikosi cha Simba chini ya miaka 20 wakati bingwa wa msimu huu anapata Milioni 5 huku mshindi wa pili akipata milioni tatu na mshindi wa tatu milioni mbili pesa zitakazotolewa na mdhamini wa michuano hiyo kampuni ya Azam kupitia Maji ya UHAI.

Msemaji wa Shirikisho la soka nchini Clifford Ndimbo amethibitisha kuhusu Maandalizi kukamilika na tayari timu na viongozi wako njiani kwenda Dodoma.

Haya hapa makundi ya michuano hiyo


Kundi A

Yanga
Ruvu Shooting
Mbeya City
Mbao FC

Kundi B

Simba
Singida United
Stand United
Njombe Mji

Kundi C

Azam FC
Mtibwa Sugar
Mwadui FC
Majimaji

Kundi D

Tanzania Prisons
Lipuli FC
Kagera Sugar
Ndanda

Makundi hayo yamepangwa kulingana na jinsi timu zilivyo maliza ligi msimu uliopita ambapo zile nne za juu zimeongoza makundi hayo.

No comments

Powered by Blogger.