NDOTO ZA SINGIDA UNITED KUCHEZA FAINALI SUPER CUP ZAYEYUSHWA NA GOR MAHIA

Mabingwa watetezi wa michuano ya SportPesa Super Cup msimu uliopita Gor Mahia ya Kenya imefanikiwa kutinga katika fainali za michuano hiyo mwaka huu ikiitupa nje Singida United katika mchezo wa nusu fainali ya pili kwa kuitandika bao 2-0.

Matokeo hayo yanawafanya Gor Mahia kutinga fainali ambapo watakutana na wekundu wa Msimbazi Simba ambao ambao waliwafunga KK Homeboyz kwa penati 5-4 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza mapema mchana wa leo.

Mchezo wa fainali ya michuano hiyo utapigwa siku ya Jumapili saa 9 alasiri ukitanguliwa na mchezo wa  mshindi wa tatu Kati ya Kakamega dhidi ya Singida United.

 Ladha ya mchezo huo ilipungua hasa kipindi cha kwanza kutokana na mvua kubwa kunyesha na kupelekea uwanja kujaa maji.

 Mabao yote ya Gor Mshia ambao pia ni mabingwa wa soka Kenya yalifungwa na Meddy Kagere dakika za 37 na 88 mabao ambayo yanawapa nafasi Gor Mahia kutetea ubingwa wao.

 Kagere ambaye aliikuwa mfungaji bora wa michuano iliyopita iliyofanyika mwaka jana jijini Dar es Salaam na ndiye kinara wa ufungaji mpaka sasa akiweka kambani mabao matatu.

Gor Mahia inafundishwa na kocha mkuu wa zamani wa Simba Dylan Kerr na mchezo wa fainali unategemewa kuwa wa upinzani mkali kwani licha ya kuwa bingwa lakini mshindi atapata nafasi ya kwenda kucheza mechi dhidi ya Everton ya England katika maandalizi ya Msimu mpya wa ligi kuu ya England.

No comments

Powered by Blogger.