KOCHA MFARANSA WA SIMBA "ATIMULIWA"
Habari zisizo rasmi kutoka Kwa mabingwa wa ligi kuu Soka Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba zinasema kwamba kocha wake mkuu Mfaransa Pierre Lechante ametimuliwa ndani ya klabu hiyo.
Chanzo cha kuaminika toka ndani ya klabu hiyo kinasema Lechante amekataliwa kuongeza mkataba wa kuinoa klabu hiyo kongwe licha ya kuipa ubingwa bila kupoteza mchezo wowote baada ya kusota Kwa takribani miaka mitano.
Mkataba Kati ya Simba na kocha huyo ulikuwa ni wa miezi 6 baada ya hapo ndipo mazungumzo mengine yangefanyika lakini inasemekana kwamba Uongozi haujaridhiswa naye hali iliyopelekea kutompa mkataba mpya.
Simba iko Nchini Kenya katika mashindano ya SportPesa Super Cup na mchana huu inacheza dhidi ya KakaMega FC ya Kenya katika hatua ya nusu fainali na hata katika bechi la ufundi Leo yuko kocha msaidizi Masoud Djuma.

No comments