SIMBA YAINGIA NUSU FAINALI SPORTPESA YAITOA SHARKS KWA PENATI

Mabingwa wa Tanzania bara timu ya Simba imeingia fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Kariobangi Sharks kwa mikwaju ya penati 3-2.

Mlinda mlango Aishi Manula alicheza mikwaju miwili ya penati huku moja ikigonga mwamba.

Kiungo Jonas Mkude ndiye aliyefunga penati ya tano na ushindi iliyoipeleka Simba hatua hiyo ambayo watakutana na Kakamega Homeboyz ambayo iliwatoa Yanga.

Penati nyingine za Simba zilifungwa na Haruna Niyonzima na Erasto Nyoni wakati Mohammed Hussein na Paul Bukaba wakipoteza mikwaju yao.

Mchezo huo ulienda katika hatua ya penati baada ya kumalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye muda wa kawaida.

Licha ya kuingia nusu fainali Simba haikucheza soka safi kama ilivyotegemewa na wengi kitu ambacho kocha Pierre Lechantre anapaswa kulifanyia kazi haraka.

No comments

Powered by Blogger.