MOROCCO KURITHI MIKOBA YA HANS SINGIDA UNITED
Kitendawili cha nani atabeba mikoba ya Hans van der Pluijm Pale Singida United kimeteguliwa leo rasmi baada ya mechi fainali ya kombe la shirikisho (ASFC).
Kocha Hans ambaye amekinoa kikosi cha Singida United kwa msimu mmoja alitangazwa kujiunga na wanalambalamba wa Chamazi klabu ya Azam FC.
Baada ya mechi ya fainali ambapo Singida Wamelazwa na Mtibwa Sugar kwa mabao 3-2, Singida United walichukua nafasi hiyo kumtambulisha kocha mpya atakayebeba mikoba ya Hans naye si mwingine bali ni Hemedi Ally Morocco.
Hemedi Morocco anakubwa vizuri baada ya kufanya vizuri na timu ya taifa ya Zanzibar na kuifikisha fainali ya CECAFA nchini Kenya japo walifungwa na Wenyeji Kenya kwa mikwaju ya Penati zilizofanyikwa mwezi desemba 2017
No comments