HATMA YA GRIEZMANN KUJULIKANA KABLA YA KOMBE LA DUNIA

Mshambuliaji nyota wa Atletico Madrid Antoine Griezmann amesema atatangaza mustakabali wake wa soka kwa msimu ujao kabla ya michuano ya kombe la dunia huko Urusi kuanza.

Image result for GRIEZMANN FRANCE 2018

Griezmann, raia wa Ufaransa ambaye aliiwezesha timu yako ya Atletico Madrid kutwaa kombe la Europa akifunga mabao mawili katika mchezo wa fainali dhidi ya Marseille amekua akihusishwa sana na uhamisho wa kujiunga na Barcelona.


Akihojiwa jana kama kuna lolote kuhusu 'future' yake litakalotangazwa hivi karibuni,  baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia ambao Griezmann ambaye aliifungia timu yake ya taifa ya Ufaransa bao moja kwa mkwaju wa penati alisema ni kweli mustakabali wake utatangazwa mapema kabla ya michuano hiyo kuanza.

No comments

Powered by Blogger.