MTIBWA SUGAR WABABE WA KOMBE LA SHIRIKISHO 2017/18
![]() |
Ismail Mhesu Mfugaji wa goli la Ushindi la Mtibwa Sugar |
Timu ya soka ya Mtibwa Sugar imeibuka wababe wa kombe la shirikisho kwa msimu huu. Mtibwa Sugar imepata ubingwa huu baada ya kuilaza Singida United kwa jumla ya magoli 3-2.
Goli la kwanza la Mtibwa lilifungwa na Salum (22') Aliyepiga shuti kali liliomshinda mlanda lango wa Singida United. Goli la pili la Mtibwa Liliwekwa kimiani na Issa Rashid kwa mpira wa kona uliyopigwa na kuingia moja kwa moja langoni.
Singida Waliendelea kulisakama lango la Mtibwa na kufanikiwa kufunga goli la kwanza dakika ya 43 goli liliofungwa na Salum Chuku na kufunya mchezo huo wa fainali kwenda mapumziko Mtibwa Sugar wakiwa mbele kwa 2-1
Kipindi cha pili Singida Untied waliingia kwa kasi na dakika ya 70 Tafadzwa Kutinyu akaisawazishia Singida United kwa kufunga goli la pili baada ya safu ya ulinzi na kipa wa Mtibwa kukosa mawasiliano mazuri baina yao
Mchezo uliendelea huku timu zote zikitafuta goli la ushindi lakini dakika ya 79 beki wa Mtibwa Sugar na Mfungaji wa goli la pili Issa Rashid maarufu kama Baba Ubaya Anatolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi mbili za njano.
![]() |
Issa Rashidi wa Mtibwa Sugar akitoka nje baada ya kupewa kadi nyekundu |
Dakika ya 87 Mtibwa wanapata bao maridadi kupitia kwa Ismail Mhesa, bao linalodumu mpaka kipenga cha mwisho na kuwafanya Mtibwa Sugar Kutangazwa rasmi mabingwa wa Kombe la Shirikisho na ndiyo watakuwa wawakilishi wetu katika kombe la shirikisho Barani Afrika.
Kiungo Hassan Dilunga amechaguliwa mchezaji bora wa mashindano wakati Habib Kiyombo akiwa mfungaji bora huku Mhesa akipata tuzo ya mchezaji bora wa mechi 'man of the match'.
Hongera kwao wamestahili.
ReplyDelete