JEZI ZA NIGERIA KOMBE LA DUNIA ZAPAGAWISHA


Ilibidi mashabiki na wapenzi wa soka hasa waafrika waishio London wasubiri kwa hamu sana nje ya duka kubwa la kampuni ya Nike lililopo katika mitaa ya Oxford ili kununua jezi mpya za Nigeria zilizozinduliwa leo ambazo zitatumika katika fainali za kombe la dunia mwaka huu.

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike imeanza kuuza jezi hizo pamoja na zile za mazoezi ambazo Nigeria inayoshiriki michuano ya kombe la dunia kwa mara ya sita itazitumia huko Urusi.

Katika uzinduzi huo wameshiriki mastaa kama Wizkid, Grace Ladoja, Julie Adenuga kwa pamoja na mastaa wa soka kama Alex Iwobi, Wilfred Ndidi, na Kelechi Iheanacho ambao wameonekana katika picha ya pamoja wakiwa wamevalia 'nyuzi' hizo

Jezi hizo zimeisha kwa muda mchache sana huku mamia ya wapenzi na mashabiki wakiwa wamekosa

No comments

Powered by Blogger.