LOW KUWAPUMZISHA MATS HUMMELS NA MULLER DHIDI YA AUSTRIA KESHO

Image result for hummels muller
Mats Hummels na Thomas Muller hawatocheza mchezo wa kujipima ubavu wa timu ya taifa ya Ujerumani dhidi ya Austria baada ya kocha Joachim Low kuamua kutumia wachezaji ambao bado hawajajihakikishia nafasi ya kujumuishwa katika kikosi kitakachoelekea Urusi kwa ajili ya fainali za kombe la dunia.


Mabingwa hao watetezi watacheza mchezo huo wa kwanza wa kujipima nguvu katika jiji la Klagenfurt kesho Jumamosi huku ikielezwa kuwa kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 cha Ujerumani kitatangazwa mapema juma lijalo.

Wakati huu ambao bado Low hajakipata kikosi chake kamili, amesema hakuna sababu ya kuwajaribu tena wachezaji wake muhimu walioshiriki kikamilifu kufuzu kwa michuano hiyo kwani wengi wao wamechoka kutokana na majukumu mazito katika vilabu vyao.

Mlindamlango Manuel Neuer anatarajiwa kuwepo langoni baada ya kurejea karibuni kutoka kwenye majeraha huku Marco Reus pia akitaraji kupata nafasi lakini Hummels na Muller wao watapumzika.

No comments

Powered by Blogger.