NDAYIRAGIJE KOCHA MPYA KMC

Aliyekuwa kocha wa Mbao FC,  Ettiene Ndayiragije ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

Raia huyo wa Burundi amechukua mikoba ya Fred Minziro aliyeipandisha timu hiyo daraja ambapo anatarajiwa kupangiwa majukumu mengine.

Ndayiragije anakumbukwa kwa kuifikisha Mbao fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup msimu wa 2016/17 ambapo walipoteza mbele ya Simba.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Benjamin Sitta ndiye aliyemtambulisha kocha huyo ambapo amesema wameridhishwa na rekodi nzuri ya raia huyo wa Burundi ambaye wanaamini ataisaidia kufika mbali.

"Nachukua nafasi hii kumtambulisha kocha Ettiene kuwa kocha mkuu wa KMC kuanzia msimu mpya wa ligi, bodi imeridhishwa na uwezo mkubwa wa kocha na tunaamini atatufikisha mbali," alisema Mstahiki Meya.

Meya sita amesema wameingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha ambaye wana matarajio makubwa nae.

No comments

Powered by Blogger.