YANGA YALIA KUINGIZWA MJINI NA NGOMA.

Kitendo cha mshambuliaji Donald Ngoma kujiunga na Azam FC kimeiumiza kwa namna fulani timu yake ya zamani ya Yanga wakiamini hajawatendea haki.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo, Hussein Nyika ameeleza masikitiko yake baada ya Ngoma kutambulishwa jana kama mchezaji mpya wa Azam.

Mwenyekiti huyo amesema kilicho waumiza zaidi ni kujiunga na wapinzani wao ndani ya ligi huku wao wakimvumilia kwa muda wote alipokuwa majeruhi.

Nyika amesema bado walikuwa na mipango na raia huyo wa Zimbabwe lakini hajafanya uungwana kwa kuamua kutimka ghafla.

"Naweza kusema Ngoma hajafanya kitendo cha kiungwana hata kidogo, nimeumizwa kwa kitendo chake cha kuondoka na kuhamia klabu nyingine, yote kwa yote namtakia kheri huko alipohamia," alisema Nyika.

Wakati huo huo Nyika amesema wapo kwenye mchakato wa kutafuta mbadala wa mshambuliaji huyo ambaye alikuwa kipenzi cha Wana Yanga.

No comments

Powered by Blogger.