RONALDO AASHIRIA MWISHO WA ENZI YAKE REAL MADRID



Nyota wa Real Madrid, Mreno Christiano Ronaldo amesherehekea taji lake la nne la ligi ya mabingwa ulaya ndani ya misimu mitano iliyopita ndani ya klabu yake huku akiashiria kwamba muda wake wa kuwepo Bernabeu umefikia tamati.


Ronaldo ambaye sasa ametwaa makombe matano ya ubingwa wa Ulaya amesema maneno ambayo yanatilia shaka uwepo wake akisema "Imekua vema kuwa ndani ya Real Madrid, ndani ya siku chache zijazo nitazungumza. Nitafurahia mafanikio haya na wenzangu kisha nitatoa majibu"


"Tumeweka historia, hilo ndiyo jambo muhimu, 'future' ya mchezaji si muhimu." Alisema Ronaldo.

No comments

Powered by Blogger.