KICHUYA KUTIMKA? SIMBA YAMUANDAA MBADALA WAKE


Moja kati ya habari zisizopendeza masikioni mwa mashabiki wa mabingwa wapya wa soka Tanzania Bara Simba kwa sasa ni hii ya kiungo wao Shiza Kichuya kutimka klabuni hapo.


wapendasoka.com inafahamu kuwa Simba tayari wamefanya mazungumzo ya awali na nyota wa Majimaji Marcel Boniventure Kaheza kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo huku tetesi zikienea kuwa ni kwa ajili ya kuziba pengo la Kichuya ambaye anaweza kuondoka wakati wowote.

Kichuya mwenyewe ameshindwa kukubali wala kukataa kwamba atakuwepo Simba msimu ujao huku akidai kuwa baba yake amekua akimhimiza kutafuta maisha zaidi nje ya nchi,

“Suala la mkataba mpya na Simba siwezi kuliongelea kwa sababu bado sijamaliza mkataba wa kwanza hadi hapo utakapokwisha nitaweka wazi, kweli baba yangu amesema nikacheze nje ni sawa kwa sababu ni maoni yake kama mzazi maana anaona akina Simon Msuva, Mbwana Samatta na Abdi Banda wakifanya vizuri nje.

“Najua hilo limekuwa likimuumiza lakini hata mimi napambana kufanya vizuri ili niweze kupata nafasi ya kwenda kucheza nje na hilo ndiyo lengo kubwa la kujituma kwa sababu nataka kuondoka hapa nilipo na wakati wowote kutoka sasa iwapo mipango yangu itafanikiwa kwenda vizuri,” alisema Kichuya.

No comments

Powered by Blogger.