YANGA WAUVUTA NYUMA MKUTANO WAO.
'Ngoja ngoja yaumiza matumbo' ndiyo msemo sahihi unaoweza kutumika hapa baada ya Yanga kuurudisha karibu mkutano wao mkuu ambao hapo awali walipanga kuufanya June 17 na sasa wameamua kuufanya Jumapili ya June 10.
Mahali utakapofanyika mkutano huo patatangazwa japo awali ulipangwa ufanyike katika bwalo la maafisa wa Polisi na wapendasoka.com inajua kuwa taratibu zinafanyika ili ufanyike hapo hapo.
Taarifa maalum toka Yanga imesema kuwa wanachama watakaoshiriki katika mkutano huo ni wale wenye kadi (mpya na za zamani) ambazo zimelipiwa lakini pia ni lazima mwanachama awepo kwenye register ya klabu na ile ya tawi lake.
Wana yanga wamekua na hamu kubwa na mkutano huo kutokana na kusuasua kwa mwenendo wa klabu yao katika siku za karibuni, hali iliyopelekea kuvuliwa ubingwa wao wa soka Tanzania bara waliouhifadhi kwa misimu mitatu mfululizo.
Awali kabisa mkutano huu ulipangwa kufanyika mapema mwezi Mei lakini ukapelekwa mbele hadi Juni 17 kutokana na Yanga kukabiliwa na ratiba ngumu ya mashindano lakini sasa umerejeshwa hadi Juni 10.
No comments