BAADA YA 'MABOKO' KARIUS AWAANGUKIA WAPENZI WA LIVERPOOL.
Mlinda mlango wa Liverpool Loris Karius ameomba radhi kwa familia nzima ya Liverpool baada ya kufanya makosa mawili makubwa katika mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya yaliyowagharimu pakubwa majogoo hao wa Anfield.
Katika usiku huo mchungu kwa Karius, Real Madrid walifanikiwa kunyakua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya Gareth Bale akitokea bench kupachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1.
Makosa mawili ya Karius yalikua na mchango mkubwa katika kipigo hicho cha Liverpool hasa katika goli la kwanza baada ya mjerumani huyo kwa bahati mbaya kuurusha mpira uliozuiliwa na Karim Benzema mapema kipindi cha pili na kutinga moja kwa moja wavuni kuiandikia Real Madrid bao la kwanza.
Bale alipiga 'tikitaka' safi iliyowatanguliza tena Madrid kwa mabao 2-1 ikiwa ni baada Sadio Mane wa Liverpool kusawazisha makosa ya Karius kwa bao lililotokana na mpira wa kona.
Lakini jinamizi halikumwacha Karius kwani aliruhusu tena kuponyokwa na mpira kutoka mbali uliopigwa na Bale na kuiandikia Real Madrid bao la tatu.
Karius alibubujikwa na machozi baada ya kipyenga cha mwisho huku akikubali kubeba mzigo wa lawama kwa kipigo hicho, "Sihisi chochote sasa hivi, leo nimeigharimu timu yangu mchezo, naomba radhi kwa watu wote, naomba radhi kw wote, kwa timu na klabu kwa ujumla kwa makosa yaliyotugharimu leo"qQ

![]() |
Karius alimuangushia mpira Karim Benzema |

No comments