UNAI EMERY AMTAJA NEYMAR SABABU YA KUONDOKA PSG


Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery amemtaja Mchezaji ghali kabisa Duniani Neymar kama ndiye sababu kubwa ya yeye kuamua kuondoka katika klabu ya PSG.


Unai Emery aliachana na PSG Mara tu baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Ufaransa mwaka 2017/2018 akidumu na klabu hiyo Kwa misimu miwili pekee.

Unai ametaja usajili wa Neymar kutoka Barcelona ulibadilisha kabisa jinsi ya mambo yalivyokuwa yanaendelea katika klabu hiyo ambao ni Mabingwa wa Ufaransa.

"Tofauti na Manchester City ambapo Pep ndiye huamua mchezaji yupi hucheza PSG baada ya ujio wa Neymar yeye ndiye aliyekua akiamua anataka acheze mechi ipi na hata kufikia kuchagua Baadhi ya mechi za yeye kuanza Ili awe salama kwaajili ya kuitumikia Brazil kwenye kombe la dunia" Alisema Unai.

Unai aliamua kujiweka pembeni na tayari ameshapata sasa nafasi ya kuifundisha Arsenal akichukua nafasi ya Arsene Wenger.

No comments

Powered by Blogger.