MAKOSA YA KIPA LIVEPOOL YAIPA REAL MADRID UBINGWA, SALAH AUMIA
Real Madrid wamefanikiwa kutetea ubingwa wao wa ligi ya Mabingwa barani Ulaya Kwa Mara ya tatu mfululizo baada ya kuwafunga Liverpool bao 3-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa jijini Kyiev Nchini Ukraine.
Mchezo huo ulianza Kwa Liverpool kutawala vilivyo dakika za mwanzo za mchezo huo mpaka dakika ya 31 wakati Mohamed Salah alipotoka baada ya kuumia bega na kuanzia muda huo kibao kikawabadilikia Liverpool na waliruhusu kushambuliwa vilivyo na mpaka Mapumziko hakuna aliyefanikiwa kupata bao.
Makosa ya mlinda mlango wa Liverpool Karius yaliwapa Real Madrid magoli mawili bao la kwanza likifungwa na Karim Benzema akiuwahi mpira ambao Karius alipotaka kumwanzishia beki wake na bao la tatu lililofungwa na Gareth Bale dakika ya 83 Kwa shuti hafifu ambalo kipa huyo alishindwa kudaka na mpira kuzama kimiani.
Bale aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Isco dakika ya 61 na ndiye aliyefunga pia bao la pili kwa tikitak.
Huu ni ubingwa wa 13 kwa Real Madrid katika maahindano hayo makubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya na ni Mara ya tatu mfululizo Real Madrid wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo.
Mchezo huo ulianza Kwa Liverpool kutawala vilivyo dakika za mwanzo za mchezo huo mpaka dakika ya 31 wakati Mohamed Salah alipotoka baada ya kuumia bega na kuanzia muda huo kibao kikawabadilikia Liverpool na waliruhusu kushambuliwa vilivyo na mpaka Mapumziko hakuna aliyefanikiwa kupata bao.
![]() |
Kipa wa Liverpool Karius akiangalia mpira wa Benzema ukienda Nyavuni |
Makosa ya mlinda mlango wa Liverpool Karius yaliwapa Real Madrid magoli mawili bao la kwanza likifungwa na Karim Benzema akiuwahi mpira ambao Karius alipotaka kumwanzishia beki wake na bao la tatu lililofungwa na Gareth Bale dakika ya 83 Kwa shuti hafifu ambalo kipa huyo alishindwa kudaka na mpira kuzama kimiani.
![]() |
Mchezaji bora wa mechi Gareth Bale alieingia Kutoka benchi na kufunga goli mbili |

No comments