SOUTHGATE AMTEUA HARRY KANE NAHODHA MPYA UINGEREZA


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amemtangaza Mshambuliaji  wa  Tottenham Harry Kane  kuwa nahodha mpya wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza  kitakacho shiriki michuano ya kombe la dunia itakayo anza mwezi ujao nchini Urusi.

Southgate ametangaza maamuzi hayo  leo kupitia vyombo vya habari huku zikiwa zimebaki siku 22 kuanza kwa michuano hiyo mikubwa duniani kwa ngazi ya mataifa

" Harry ni kiongozi mzuri ndani na nje ya timu na ana sifa zote za kuwa kiongozi ," alisema Soughagate.

Wiki iliyopita mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya uingereza Frank Lampard alimpigia chapuo Harry Kane kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza

No comments

Powered by Blogger.