MANAHODHA WA NCHI PINZANI WAUNGANA KUMUOMBEA MWENZAO AFUNGULIWE NA FIFA

Image result for PERU WORLD CUP
Kuelekea fainali za kombe la dunia zinazotarajiwa kuanza kurindima mwezi ujao, nahodha watatu kutoka kundi c linalojumuisha nchi za Ufaransa, Peru, Denmark na Australia wameungana na kuiandikia FIFA barua yenye lengo la kuomba FIFA wamruhusu nahodha Paolo Guerrero wa Peru acheze kombe la dunia.

Guerrero amekumbwa na kifungo cha kutojihusisha na soka cha miezi 14 baada ya vipimo kuonesha anatumia dawa za kulevya aina ya cocaine.

Dawa hizo zinasemekana ziliwekwa kwenye chai aliyokunywa Guerrero na manahodha hao wanadai kuwa Guerrero alikunywa chai hiyo bila kuja kama imewekewa cocaine

Katika barua hiyo wanaeleza "tunaamini kuwa hukumu ikilegezwa kwa muda itakuwa ni jawabu tosha kwa Paolo na Peru"

Hukumu hiyo kwa Paolo imeamsha hisia tofauti katika mitaa mbalimbali nchini Peru, wananchi wamekusanyika katika maeneo mbalimbali wakijaribu kuishinikiza FIFA imruhusu Nahodha Wao na Mfungaji Wao aweze kucheza fainali hizo.

Raisi wa taifa la Peru ameiingilia kati na kuiagiza serikali kumsaidia Paolo Guerrero ili kuhakisha anacheza kombe la Dunia mwezi ujao

Hebu angalia kipande hiki hapa chini huu ukiwa ni mkusanyiko wa wananchi wa peru katika uwanja wa mpira wa Estadio Nacional.







No comments

Powered by Blogger.