HUYU HAPA MRITHI WA WENGER PALE ARSENAL
Arteta mwenye umri wa miaka 36 alionekana kuwa
tayari kutwaa mikoba hiyo baada ya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Arsenal
huku akiwa ni chaguo la CEO Ivan Gazidis lakini inaonekana kama maamuzi
yamebadilika mwishoni.
Emery mwenye umri wa miaka 46 aliachana na
PSG ya Ufaransa mwishoni mwa msimu wa 2017/18 akiwa ameshinda kombe moja la la
Ligue 1, vikombe viwili vya Coupes de France, viwili vya Coupe de la Ligue
pamoja na viwili vya Supercup katika misimu miwili aliyodumu hapo.
Emery alisafiri hadi London jana Jumatatu kwa
ajili ya mazungumzo lakini www.wapendasoka.com inatambua kuwa alifanya
mazungumzo pia na West Ham lakini iwapo mambo yatamwendea vema na Arsenal basi
atasaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.
No comments