SOKA LA VIJANA MKOANI IRINGA LAPIGWA JEKI

Kampuni za Alishati Investment na Puma Energy wamejitokeza kudhamini kituo cha kukuzia vijana cha mkoani Iringa (Iringa Football Academy).

Alishati atakuwa mfadhili wakati Puma ni mdhamini ambaye atatoa vifaa kwa ajili ya mechi na mazoezi pamoja na kugharamia mafuta ya usafiri kwa mechi za ugenini.

Udhamini huo utakiwezesha kituo hicho kufanya kazi kwa weredi na kuzalisha wachezaji wazuri ndani ya mkoa wa Iringa.
Mkurugenzi Mtendaji wa IFA, Ally Msigwa
Mkurugenzi Mtendaji wa IFA, Ally Msigwa amemtangaza Kocha Mshindo Msola kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa kituo hicho.

Mkurugenzi huyo pia ametangaza wajumbe saba wa bodi ya IFA akiwemo Waziri wa mambo ya nje Dk. Augustino Mahiga.

No comments

Powered by Blogger.