LUKAKU HATIHATI KUIKOSA BRIGHTON


Mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku anaweza akakosa mchezo wa ligi kuu ugenini dhidi ya  Brighton siku ya Ijumaa.

Kinara huyo wa mabao ya United alipata maumivu ya enka katika mchezo dhidi ya Arsenal wikiendi iliyopita uliomalizika kwa ushindi wa  2-1 Old Trafford.

Raia huyo wa Ubelgiji alifanyiwa vipimo jana Jumatatu na sasa anasubiri majibu ili kuona kama ameumia kwa kiasi gani.

Meneja wa United, Jose Mourinho amesema kama Lukaku atakuwa hajaumia sana atarejea uwanjani mapema.

"Sijui ameumia kwa kiasi gani, sidhani kama atakuwa nje ya uwanjani kwa muda mrefu, anapenda kucheza muda wote.

 “Lukaku hachoki, na kama jeraha litakuwa ni dogo hajali anarudi mazoezini, nilimfanyia mabadiliko sababu alishindwa kucheza," alisema Mourinho.

No comments

Powered by Blogger.