LICHA YA KUFUNGWA LIVERPOOL YATINGA FAINALI MABINGWA ULAYA 



Mechi ya marudiano ya nusu fainali katika ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya Wenyeji AS ROMA na Liverpool imemalizika Kwa Wenyeji Roma kuibuka na ushindi wa bao 4-2.

Licha ya Kipigo hicho bado Liverpool imeweza kutinga katika hatua ya fainali ya michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya Kwa ushindi wa jumla wa bao 7-6 baada ya mechi ya awali kumalizika kwa Liverpool kushinda bao 5-2.

Makosa ya Safu ya Ulinzi ya Roma yaliiwezesha Liverpool kupata bao la lililofungwa na Sadio Mane dakika ya 9 ya mchezo lakini ilipofika dakika ya 15 ya Mchezo Roma walifanikiwa  kupata bao la kusawazisha baada ya James Milner kujifunga na kisha Gergio Wijnaldum akaongeza bao la pili kwa mpira wa kichwa na  mpaka mapumziko Liverpool walikua mbele Kwa bao 2-1.

 Dakika ya 52 Edin Dzeko aliisawazishia Roma bao la pili kisha Radja Nainggolan akaongeza mengine mawili kufanya mchezo huo kumalizika Kwa ushindi huo wa bao 4-2 Kwa Roma.

Liverpool watacheza dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Real Madrid katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Olympic jijini Kyiv Ukraine Tarehe 26 mwezi huu.

No comments

Powered by Blogger.