YANGA KUSAFIRI KESHO KUWAFATA WAARABU
Mabingwa
wa ligi kuu na wawakilisha pekee waliosalia katika michuano ya kimataifa Yanga wanatarajia
kuondoka nchini kesho Mei 3 kuelekea nchini Algeria kwa ajili mchezo wa kwanza
wa makundi wa kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.
Msemaji wa klabu ya Yanga, Dismas
Ten amesema wameamua kuondoka siku tatu kabla ya mchezo ili wachezaji kuzoea
mazingira na mwisho wa siku wapate ushindi.
Yanga itaondoka Alhamisi kuelekea
Algeria ikipitia Dubai kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya USM
Alger siku ya jumapili tarehe 6
Yanga iko kundi D ikiwa na Gor
Mahia ya Kenya, Rayon Sports ya Rwanda, pamoja na USM Alger
No comments