MICHUANO YA SPORT PESA, SIMBA NA YANGA KUVAMIA NAIROBI KESHO

Miamba ya soka Tanzania Simba na Yanga hapo kesho inatarajia kuondoka nchini kwa nyakati tofauti kuelekea nchini Kenya kushiriki michuano maalum ya vilabu vinavyodhaminiwa  na kampuni ya Sport Pesa hapa Afrika Mashariki.

Simba wao tayari wameweka wazi kwamba wataondoka saa moja asubuhi na ndege ya shirika la KQ wakiwa na kikosi chao kizima kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanaibuka na kikombe hicho.


Kwa upande wa Yanga wao inafahamika kwamba wataondoka kesho na kikosi cha wachezaji 20 tu ambao watafahamika leo hii.

Michuani hiyo ilifanyika kwa mara ya kwanza mwaka jana hapa nchini na klabu ya Gor Mahia kuibuka mabingwa na kujipatia fursa ya kucheza na Everton ya Uingereza ndani ya ardhi ya Tanzania.

Vilabu vya Tanzania hasa Simba vimeonesha kuyapa umuhimu mkubwa mashindano hayo msimu huu zaidi ya msimu uliopita.

No comments

Powered by Blogger.