SINGIDA UNITED WASHUSHA MBRAZIL.

Klabu ya Singida United imezidi kujiimarisha katika maandalizi ya msimu ujao wa soka ambao huenda wakashiriki michuano ya kimataifa kama wataifunga Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho.

Taarifa iliyotufikia ni kwamba Singida tayari wamemsajili mshambuliaji kutoka Brazil Felipe Oliveria dos Santos ambaye tayari  amemalizana na mabosi wa Singida.

Mbrazil huyo aliwahi kuichezea Asec Mimosas ya Ivory Coast na alikipiga katika ligi ya mabingwa Afrika.

Huo ni usajili wa pili kwa klabu hiyo baada ya kuwa wamemnasa kiungo Mzanzibari Faisal Salum kutoka JKU

No comments

Powered by Blogger.