KUZIONA SINGIDA, MTIBWA BUKU TU
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa fainali wa michuano ya Azam Sports Federation Cup ambapo cha chini kitakuwa shilingi elfu moja.
Mchezo huo wa fainali utazikutanisha timu za Singida United na Mtibwa Sugar siku ya Jumamosi mtanange utakaopigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo ametangaza viingilio hivyo kuwa ni sh 1000 kwa mzunguko, sh 2000 kwa geti B na C wakati VIP itakuwa sh 10,000.
Bingwa wa michuano hiyo atapata kikombe pamoja kitita cha sh milioni 50 mshindi wa pili atapata sh milioni 10 ambapo msimu uliopita hakukuwa na zawadi.
Mbali na zawadi hizo kutakuwa pia tuzo ya mchezaji bora wa fainali, mchezaji bora wa michuano, kipa bora na mfungaji bora.
"Tumeamua kuweka viingilio vya bei ya chini ili kuiwawezesha mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi," alisema Ndimbo.

No comments