KUTINYU HUYOOO AZAM FC

Image result for kutinyu

Harakati za usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa soka Tanzania bara zimezidi kupamba moto na sasa habari iliyopo inamhusu mshambuliaji wa Singida United ya Singida, Tafadzwa Kutinyu kutimka klabuni hapo.


Taarifa ambazo www.wapendasoka.com imezipata ni kwamba Mzimbabwe huyo anaelekea Azam FC baada ya kushawishiwa na kocha wake Hans Van der Pluijm ambaye pia ametimkia kwa wanalambalamba hao.

Inaelezwa kuwa Kutinyu alikua kwenye rada za Simba ambao walikua wakihitaji huduma yake lakini ushawishi wa kocha ambaye ndiye aliyemleta Singida umekua na nguvu zaidi.

Iwapo dili hili litakamilika, huenda Azam wakawa na safu kali ya ushambuliaji itakayoundwa na wazimbabwe wawili ambao ni Kutinyu na Donald Ngoma.

No comments

Powered by Blogger.