AWAMU YA PILI YA SPORTPESA SUPER CUP KUZINDULIWA
Awamu ya pili na mashindano yanayohusisha timu bora za Afrika
Mashariki-SportPesa Super Cup yanatarajiwa kuanza Juni 3-10, 2018 nchini Kenya
kwenye uwanja wa Kimataifa wa Moi uliopo Kasarani.
Timu zitakazoshiriki katika michuano
hiyo kutoka Tanzania ni timu zinazodhaminiwa na SportPesa ambazo ni Simba,
Yanga, Singida United pamoja na JKU (Jeshi la Kujenga Uchumi kutoka Zanzibar),
wakati kutoka Nairobi timu zitakazoshiriki ni Gor Mahia, AFC Leopards na
Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi za SportPesa zilizopo Masaki, Dar es Salaam ambapo pia walikuwepo
wawakilishi na viongozi kutoka TFF pamoja na viongozi wa timu za Simba, Yanga
na Singida United Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Bwana Tarimba Abbas alisema
“michuano hii kuleta chachu na kumpata bingwa kwa upande wa Africa Mashariki”
“Matayarisho ya mwaka huu yamefanyika
mapema na ukiangalia muda wa kupewa na taarifa mpaka kuanza ni zaidi ya mwaka
mmoja, hivyo basi hakuna sababu kwa timu zetu za Tanania zisifanye vibaya zaidi
ya mwaka jana kwani matayarisho yamefanyoka mapema na kwa hali hiyo timu zikifanya
vibaya tutakuwa na sababu za kuwalaumu”
“Kutakuwa na jumla ya timu nane za
Afrika Mashariki na mshindi wa michuano hiyo atacheza na moja kati ya timu
iliyoshiriki ligi kuu uingereza, Everton”
Timu zitakazoingia robo fainali
kwenye mashindano haya watapata kiasi cha dola za kimarekani 2,500, nafasi ya
nne timu itapata kiasi cha dola 5000, wakati nafasi ya tatu na wa pili dola
7,500 na 10,000 kila mmoja.
![]() |
Add caption |
Timu itakayoshinda itazawadiwa kiasi
cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kuchuana na timu ya Everton katika uwanja
wa Goodison Park.
“Napenda kuwatakia kila la kheri timu
zetu tatu zinazokwenda kutuwakilisha jijini Nairobi, natumaini zitatutoa
kimasomaso kwa kufanya vizuri zaidi ya mwaka jana, wataiwakilisha nchi yetu
vilivyo kwa kucheza kwa uweledi na nidhamu” alimaliza Ndugu Tarimba
Kwa
upande wa timu ya Simba Ndugu Said Tulliy alisema “Napenda
kuchukua nafasii hii kuwataarifu wanasimba kuwa tunakwenda kushiriki mashindano
kama timu shindani na si timu shiriki na tunajua mwaka jana tulipata nafasi kama
hii lakini tuliipoteza na tusingependa kitu kama hicho kijirudie. Tumeona faida
yake kutokana na jinsi wenzetu waliopita ni jinsi gani walivyofaidikakupitia
mashindano hayo”
“Kama
timu tumejiandaa na tuko tayari kuhakikisha tunalinda heshima ya Simba Sports
Club na heshima ya Tanzania, tunakwenda na kikosi kamili ili kuhakikisha
tunachukua ubingwa ili tuweze kushindana na timu iliyopangwa”
“Tunathibitisha
kuwa tutashiriki mashindano haya kwa sababu ni mashindano muhimu, tuko tayari
kwa ajili ya mashindano na timu yetu nzima na tuko tayari ya kushinda” alimaliza Ndugu Said Tulliy
“Changamoto
ya mashindano iko pale pale lakini kwa mwaka huu nia yetu kuu ni kuchukua
ubingwa ili kuleta heshima kimataifa” Charles Boniface Mkwasa Yanga
“Kwanza
napenda kuwashukuru SportPesa kwa sababu wamefanya timu yetu kujulikana kwenye
kila kona ya nchi, moja kati ya wadhamini wetu wa nguvu ambao tunajivunia sana
kutoka kampuni hii. Jambo kubwa tutakaloenda kulifanya kwenye michuano hii
kimsingi kwa mwaka huu tumeweza kushirikishwa mapema ili tuweze kujipanga sisi
kama timu lakini kikubwa zaidi ikumbukwe kuwa Singida United ni timu pekee
iliyofanikiwa kufika nusu fainali kwa hapa Tanzania na mwaka huu tunaamini
tutachukua kombe”
Kwa
watanzania na watu wa Africa mashariki tunaombawatuunge mkono timu yetu.
Ningependa kuwaomba SportPesa kuhakikisha kanuni na sheria za mpira wa miguu
zinafatwa ili michuano hii iweze kumalizika vizuri”–Shabani Mande Singida
United
Tunapenda kuwashukuru SportPesa kwa
kututambua na kutupa nafasi ya kushiriki katika michuano hii na napenda
kuwaahidi hatutawaangusha ingawa hii itakuw mara ya kwanza kushiriki.” Maalim
Masoud, Katibu wa klabu, JKU.
KUHUSU SPORTPESA SUPER CUP
SportPesa
Super Cup ni mashindano ya mwaka yanayohusisha timu bora kutoka Afrika Mashariki
kwa wiki moja mfululizo.
Lengo
kuu la mashindano hayo ni kuongeza chachu ya mpira wa miguu Afrika Mashariki na
kati, kuwapa fursa vijana kuonyesha na kufichua zaidi vipaji vyao.
Kama
kampuni yenya matawi nchi mbali mbali duniani yenye lengo la kuunganisha
wapenda soka duniani na kuonyesha maana ya mpira wa miguu kwa nchi za Afrika na
inawakilisha nini.
No comments