ARSENAL KUZUNGUMZA NA ARTETA LEO.

Arsenal wanataraji kufanya mazungumzo na Mikel Arteta leo Alhamisi kuhusu mpango wa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo kulingana na ripoti za kuaminika ambazo www.wapendasoka.com imezipata.

Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal anaongoza tetesi za makocha wanaotajwa kuchukua mikoba ya Arsene Wenger na inaelezwa kuwa iwapo ataajiriwa atakabidhiwa kitita cha £50 kwa ajili ya usajili katika majira ya joto.

Mabosi wa Arsenal wakiongozwa na afisa mtendaji mkuu Ivan Gazidis, Mkuu wa masuala ya soka Raul Sanllehi pamoja mkuu wa idara ya ajira Sven Mislintant wanataraji kuongoza mazungumzo hayo.

Inaelezwa kuwa Gazidis anamtaka kocha mkuu atakayefanikiwa kuingia vema katika mfumo wa utawala wa klabu na Arteta ambaye ni kocha msaidizi wa Manchester City chini ya Pep Guardiola anaonekana kupigiwa Chapuo.

Tayari Pep amekwishaweka wazi kwamba yupo tayari kumruhusu Arteta aondoke iwapo atapewa ofa ya kujiunga na Arsenal ambako inaelezwa kuwa ataruhusiwa kuajiri wasaidizi wake.

No comments

Powered by Blogger.