SOUTHGATE AWATOA POVU MASHABIKI KIKOSI CHA ENGLAND
Southgate amemtema Hart ambaye aliwahi kuwa golikipa namba moja wa kikosi hicho kutokana na kushuka kiwango katika klabu ya West Ham, nafasi yake ikichukuliwa na mlinda mlango wa Burnley, Nick Pope huku kiungo wa Arsenal Jack Wilshere pia akiondolewa.
Southgate ameamua kuwachagua John Stones, Kieran Trippier, Kyle Walker, Gary Cahill, Harry Maguire, Danny Rose, Phil Jones na Ashley Young katika safu ya ulinzi.
Kijana wa Fulham mwenye umri wa miaka 17, Ryan Sessegnon hajajumuishwa kwenye kikosi hicho pamoja na kuwa na msimu mzuri sana katika ligi daraja la kwanza (Championship)
Kikosi kizima cha England kipo hivi,
Walinda mlango: Jordan Pickford, Nick Pope, Jack Butland
Walinzi: Kyle Walker, Kieran Trippier, Trent Alexander-Arnold, Gary Cahill, Danny Rose, John Stones, Harry Maguire, Phil Jones, Ashley Young
Viungo: Eric Dier, Fabian Delph, Jordan Henderson, Dele Alli, Ruben Loftus-Cheek, Raheem Sterling, Jesse Lingard
Washambuliaji: Harry Kane, Jamie Vardy, Marcus Rashford, Danny Welbeck.
England wataianza kampeni yao katika kundi G kwa kuvaana na Tunisia mnamo June 18 kabla ya kuvaana na Panama June 24 na kumaliza na Ubelgiji June 28.
No comments