YANGA YAWAANGAMIZA WAHABESHI KOMBE LA SHIRIKISHO

wakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Yanga wameibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mechi yao ya kwanza hatua ya mwisho ya mtoano dhidi ya Walita Dicha ya Ethiopia.

Yanga walianza mchezo wa Leo vizuri baada ya kupata bao la mapema zaidi sekunde ya 30 tu baada ya mpira kuanza likifungwa na kiungo wake Raphael Daudi bao lililodumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili kiliwapa nguvu na ari zaidi Yanga kuongeza wigo wa ushindi na kufanikiwa kupata bao la Pili dakika ya 54 likifungwa na kichwa na Emmanuel Martin

Matokeo hayo ni faida kubwa Kwa Yanga kwani wanahitaji sare tu katika mchezo wao wa marudiano siku 10 zijazo mjini Adis Ababa Ethiopia.

Kama  Yanga watafanikiwa kushinda mechi zote mbili na kuwatoa Wahabeshi  hao basi watatinga hatua ya makundi  katika michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika ngazi ya klabu barani Afrika.

No comments

Powered by Blogger.