BAADA YA KUIFUNGA MAN CITY,POGBA AMTAJA MTU ANAYEMPA MBINU UWANJANI
Mfungaji wa magoli mawili ya Manchester United katika ushindi wa bao 3-2 walioupata jana dhidi ya Manchester City, Mfaransa Paul Pogba ametanabaisha na kumshukuru Michael Carick baada ya mchezo huo.
Pogba alifunga mabao mawili ya kusawazisha kipindi cha pili wakati Manchester City wakiwa tayari wanaongoza kwa bao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya England kwenye uwanja wa Etihad jijini Manchester.
"Michael Carick Ndiye anayenihamasisha kwenda mbele na kujitahidi kushambulia zaidi akiniambia naweza kuleta madhara kwa timu pinzani na nilijaribu hiyo katika mechi naona imefanikiwa" alisema Pogba
Vicent Kompany na Ilkay Gonduan ndiyo walioifungia Manchester City mabao yao huku Chris Smalling akifunga bao la 3 na ushindi kwa Manchester United kuipatia Manchester United Ushindi muhimu ugenini ambao umeizuia pia Manchester City kutangazwa mabingwa wapya wa EPL msimu huu.
Manchester City sasa inahitaji pointi 6 kuweza kutangazwa mabingwa wapya lakini wanaweza kutangazwa mabingwa kama watashinda kwenye mechi ijayo dhidi ya Tottenham huku wakiomba United ipoteze mchezo wake dhidi ya West Brom
No comments