MANCHESTER CITY KUTWAA BINGWA MGONGONI MWA MAN UNITED LEO?

Klabu ya Manchester City pengine leo itatawazwa rasmi kuwa mabingwa wapya wa ligi kuu ya England watakapoikaribisha Manchester City katika dimba la Etihad jijini Manchester katika mechi ya ligi kuu soka nchini England.
Ushindi dhidi ya Manchester United leo utawafanya Manchester City kufikisha pointi 87 ambazo haztiweza kufikiwa na timu yoyote ile kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kocha Jose Mourinho atakua na kibarua kipevu kuweza kuwazuia Manchester City leo akiiongoza United kupata pointi 3 zitakazoiwezesha kufikia pointi 71 katika nafasi ya pili wakati Pep Guadiola na kikosi chake pengine watahitaji kuwa waangalifu kwakuangalia mechi ya marudiano Jumanne ijayo dhidi ya Liverpool katika ligi ya mabingwa Ulaya.
Mechi nyingine kubwa leo ni baina ya wapinzani wawili wa jiji la Liverpool klabu ya Everton itakayokua nyumbani Goodson Park kuwaalika Liverpool mechi ya mapema kabisa siku ya leo
RATIBA KAMILI YA MECHI ZA LEO
- 14:30 - EVERTON vs LIVERPOOL
- 17:00 - AFC Bournemouth vs Crystal Palace
- 17:00 - Brighton vs Huddersfield
- 17:00 - Leicester City vs Newcastle United
- 17:00 - Stoke City vs Tottenham Hotspur
- 17:00 -Watford vs Burnley
- 17:00 - west Brom vs Swansea
- 19:30 - Manchester City vs Manchester United
NOTE: MUDA NI KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI
No comments