YANGA KAMILI KUIKABILI DICHA KESHO

Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Shirikisho Afrika timu ya Yanga ipo kamili nchini Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Wolaita Dicha ukaofanyika kesho katika mji wa Hawassa.

Katika mchezo wa kesho Yanga itahitaji ushindi wowote, sare au kufunga bao moja ili kuvuka hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika hapa nchini.

Mjumbe wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo, Ahmed Islam amesema wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wanaendelea na maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho.

Wachezaji Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa na Said Makapu ambao walikosa mchezo wa kwanza kutokana na kutumikia adhabu ya kadi wamerejea na kesho wanatarajia kuwepo kikosini.

"Wachezaji wana morali ya hali ya juu na maandalizi ya mchezo yamekamilika kikubwa tunahitaji dua za Watanzania ili tuingie hatua ya makundi, benchi la ufundi litaamua nani aenze kwakua nyota wote wako vizuri," alisema Islam.

Katika mchezo wa kesho Yanga itawakosa Ibrahim Ajib na Andrew Vincent 'Dante' ambao hawakusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi.

No comments

Powered by Blogger.