KOCHA WA PRISONS ALIA NA PENATI YA OKWI

Kocha wa Tanzania Prisons Abdallah Mohammed amelalamikia bao la pili la penati waliopata Simba katika mchezo wa l
Jana kuwa halikuwa halali.

Kocha huyo amemtupia lawama za moja kwa moja kwa mwamuzi wa mchezo huo Shomari Lawi kuwa alifanya makusudi kuwapa Simba bao hilo kwakua alijua wangeweza kusawazisha.

Mkufunzi huyo aliongeza kuwa mshambuliji John Bocco hakuwa amefanyiwa madhambi yaliyo sababisha penati hiyo kwakua kiungo Jumanne Elfadhili alicheza mpira na wala hakumfanyia rafu.

"Lile bao la penati la Simba halikuwa halali hakuna madhambi yoyote yalifanywa pale mwamuzi aliamua kuwapa ili kumaliza mchezo," alisema Kocha Abdallah.

Bao hilo lilipatikana dakika ya 80 lililofungwa na Emmanuel Okwi na kumfanya Mganda huyo kufikisha bao la 19 kwenye ligi.

No comments

Powered by Blogger.