BARCELONA YAVUTWA "SHATI" LA LIGA



Vinara wa ligi kuu ya Soka nchini Spain klabu ya Barcelona imepoteza pointi 2 katika sare ya bao 2-2 dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wa Baladois nyumbani Kwa Celta Vigo.

Lionel Messi alianzia katika Benchi katika mechi hiyo akiingia dakika ya 60 kuchukua nafasi ya Philip Countinho wakati huo timu hizo zikiwa sare ya bao 1-1.

Osmane Dembele alitangulia kuipatia Barcelona bao la kwanza dakika ya 24 kabla ya Johnny hajaisawazishia Celta Vigo dakika ya mwisho ya Kipindi cha kwanza.

Barcelona  waliongeza bao la pili dakika ya 64 likifungwa na Paco Alcacer lakini Celta Vigo walisawazisha dakika ya 82 bao la Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas ambaye marudio ya picha za video zilionyesha mpira kumgonga mkononi na kuzama  goli.

Matokeo hayo yanaendelea kuiacha Barcelona katika nafasi ya kwanza Ikiwa na pointi 83 ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote katika la liga mpaka sasa.

No comments

Powered by Blogger.