HARRY KANE "ATUPIA" SPURS IKILAZIMISHWA SARE
Mbio za ufungaji bora katika ligi kuu ya England zimeendelea kutoa matumaini Kwa Harry Kane wa Tottenham Hotspur baada ya kufunga bao lake la 26 katika sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Brighton & Hove Albion katika uwanja wa Amex.
Kane mfungaji bora Mara mbili mfululizo amebakiza mabao manne kumfikia Mohammed Salah wa Liverpool anayeongoza akiwa na mabao 30 Hivi sasa.
Spurs walitangulia kujipatia bao katika mchezo huo dakika ya 48 Kane akifunga baada ya kazi nzuri ya Hueng-Min Son lakini dakika 2 baadae Brighton walipata penati baada ya mshambuliaji wake Joze Iziquedo kuangushwa na beki wa Spurs Sergie Aurer na Paschal Gross bila ajizi akafunga penati hiyo.
Spurs wamefikisha pointi 68 katika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni huku Manchester City wakishatawazwa kuwa mabingwa wapya.

No comments