SMALLING NA LUKAKU WANG'ARISHA SHOO YA MAN UNITED UGENINI


Mlinzi wa Kati wa Klabu ya Manchester United Chriss Smalling na mashmbuliaji wa Timu hiyo Romelu Lukaku wamefunga mabao mawili na kuiwezesha United kuibuka na ushindi wa bao 2-0 ugenini dhidi ya AFC Bournemouth.

Katika Mchezo  huo pekee wa ligi kuu ya England kocha Jose Mourinho alianzisha wachezaji ambao wamekua wakikosa namba katika kikosi hicho wakiwemo mabeki wa pembeni Luke Shaw na Mateo Darmian.

Mpaka Mapumziko Tayari United walishakua mbele Kwa bao  1-0 likifungwa na Chriss  Smalling akiunganisha mpira wa krosi kutoka pembeni wa Jesse Lingard.

Lukaku aliyeingia dakika ya 62 kuchukua nafasi ya Jesse Lingard aliifungia United bao la pili dakika 8 baada ya kuingia akitumia vyema Pasi ya Paul Pogba.

Matokeo hayo yanaendelea kuiweka Man United katika nafasi ya 2 wakiwa na pointi 74 pointi 4 mbele ya Liverpool wanaokamata nafasi ya tatu.

No comments

Powered by Blogger.