RONALDO AIOKOA REAL MADRID KUCHAPWA NYUMBANI


Mchezaji bora wa dunia na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefunga bao la kusawazisha na kuiwezesha Real Madrid kuambulia sare nyumbani ya bao 1-1 dhidi ya Athletic Bilbao.

Ronaldo alifunga bao Hilo dakika ya 87 akiunganisha mpira wa Luka Modric wakati wote huo Real Madrid wakihaha kusawazisha bao la dakika ya 14 la Inaki Williams.

Matokeo mengine Valencia anafungwa nyumbani bao 2-1 dhidi ya Getafe wakati Espanyol w akafungwa 1-0 nyumbani na Eibar.

No comments

Powered by Blogger.