PAWASA AIPA NAFASI SIMBA KUIFUNGA YANGA JUMAPILI
Mlinzi wa zamani wa timu ya Simba, Boniface Pawasa
amekiri mechi ya watani wa jadi ni ngumu na haitabiliki lakini anaamini Wekundu hao wanaweza kuibuka
na ushindi mbele ya Yanga Jumapili.
Mlinzi huyo amesema Simba wapo kwenye kiwango bora
kwa sasa na wana wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote lakini
amesisitiza lolote linaweza kutokea.
Pawasa ameongeza kuwa mechi ya watani inaweza
ikakuweka katika nafasi nzuri kwenye medani ya soka lakini pia inaweza
kukupoteza kabisa katika ramani kwahiyo wachezaji wanapaswa kutambua hilo.
"Mechi ya Simba na Yanga asili yake huwa
haitabiliki ni ngumu sana, safari hii Simba ipo vizuri zaidi ya Yanga kama
wachezaji wake watacheza kwa kujituma naamini wataibuka na ushindi.
"Simba ina safu imara ya ushambuliaji ambayo
ndio imefunga mabao mengi mpaka sasa na wanajua kutengeneza nafasi ingawa
haimaanishi haiwezi kupoteza mchezo," alisema Pawasa.
Miamba hiyo itakutana Jumapili katika uwanja wa Taifa
mtanange unaotarajiwa kuanza saa 10 jioni.
No comments