ARSENAL YABANWA NYUMBANI, MARSEILLE KICHEKO EUROPA LEAGUE


Arsenal imeanza Kwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wake wa kwanza wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Europa maarufu kama Europa League dhidi ya Atletico Madrid katika uwanja wa Emirates jijini London.

 Dakika zote za kipindi cha kwanza hazikuzaa matunda licha ya Atletico Madrid kuwa pungufu kuanzia dakika ya 10 baada ya mchezaji Sime Vrsaljko kutolewa nje Kwa kadi Nyekundu kufuatia madhambi aliyoyafanya dhidi ya Alexandre Lacazette ikiwa ni kadi ya pili ya njano.

Kipindi cha Pili kila timu ilijitahidi kufunguka kupata bao na walikua ni Arsenal waliotangulia kupata bao dakika ya 61 likifungwa na Alexander Lacazette Kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi ya Jack Wilshere.


Antoine Griezman aliwanyanyua mashabiki wa Atletico Madrid akifunga bao safi na muhimu katika hatua ya kusaka nafasi ya kutinga fainali dakika ya 82 baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Arsenal ikiongozwa na Laurent Koscienly.
 Katika mechi nyingine hiyo Jana kwenye michuano hiyo Olympic Marseille wakiwa nyumbani waliifunga RB Salzburg bao 2-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutinga fainali mechi za marudiano zikitarajiwa kuchezwa Alhamis Ijayo.

No comments

Powered by Blogger.