SIMBA YATOA ANGALIZO KWA WAAMUZI MECHI YA YANGA

Klabu ya Simba imewataka waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo dhidi ya watani wao Yanga kufuata sheria 17 za soka ili mshindi apatikane kwa haki.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Hajji Manara mbele ya Waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia maandalizi ya mchezo huo utakaofanyika siku ya Jumapili.

Manara amesema wanaamini waamuzi hao watafuata sheria zote 17 za soka na kupunguza malalamiko yasio ya lazima ili mwenye haki yake apate.

"Nitoe rai kwa waamuzi waliopangwa kucheza mechi hii kufuata sheria za soka, kuna baadhi ya waamuzi huingia uwanjani wakiwa na matokeo mfukoni kitu hicho hatutaki kitokee.

"Tunataka mshindi apatikane kwa haki ambaye amestahili kushinda ndio huyo aondoke na furaha nasio vinginevyo," alisema Manara.

Mwamuzi wa kati katika mchezo huo ni Emmanuel Mwandembwa akisaidiwa na Mohammed Mkono na Frank Komba wakati mwamuzi wa akiba akiwa Heri Sasii.

No comments

Powered by Blogger.