LICHA YA FAIDA YA USHINDI MNONO WIKI ILIYOPITA, BARCELONA YAANGUKIA PUA ROMA
Barcelona iliyoingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya magoli 4-1 walizopata katika mchezo wa awali pale Nou Camp jijni Barcelona hivyo kuhitaji sare tu kuweza kuvuka kwenda nusu fainali
Edin Dzeko alitangulia kuipatia Roma bao la kuongoza dakika ya 6 tu ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko huko Roma wakionyesha kiwango bora kabisa kipindi hicho cha kwanza
Kipindi cha pili Roma walipata nguvu zaidi na kuweza kupata mabao mengine mawili huku wakizuia kutofungwa bao lolote yakifungwa mabao yao na kiungo Daniel De Rossi aliyefunga kwa penati na Konstaninos Manolas aliyefunga bao la tatu akiunganisha mpira wa kona ya Cengiz Under.
kwa matokeo hayo roma wanatinga hatua ya nusu fainali kwa faida ya goli la ugenini walilopata katika mchezo wa awali jijini Barcelona
No comments